- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANAWAKE WAFUNGUKA WADAI HAKI YA KUMILIKI ARDHI.
DODOMA: Wanawake nchini wameungana kwa pamoja katika kudai haki juu ya kumiliki Ardhi
Akizungumza katika kongamano La maadhimisho ya wanawake Wa Tanzania juu ya haki za Ardhi ambayo yamefanyika katika kijiji Makangw'a kata ya mloda Halmashauri ya wilaya ya chamwino mjini Dodoma ambapo maadhimisho hayo yamedhaminiwa na shirika la Action aid mraty afisa habari kitaifa wa ACTION AID MRATY MELEA SULUTYA amesema wanawake wanahaki ya kumiliki Ardhi kwa sababu Ardhi ni maliasili muhimu ambayo ikitumiwa vizuri inauwezo Wa kuendeleza na kuboresha hali ya Maisha ya mwanamke,kumwezesha kiuchumi na kijamii.
Sulutya amesema haki ya mwanamke kumiliki Ardhi imekuwa ni vikwanzo Vingi ukilinganisha na mwanaume kwa sababu ya kihistoria ,kijamii,kiuchumi,kiutamaduni,kidini,ambapo vingi vinambagua mwanamke kupata kumiliki na kudhibiti Ardhi.
Naye Mlatibu wa kampuni ya action aid mraty JORAM WIMMO amesema mwanamke anahaki ya kumiliiki ardhi na lasilimali Kwa sababu ardhi ni nguvu ambayo inamsaidia mwanamke kufanya shughuli mbalimbali kama kilimo ambacho kinamwezesha kujikwamuwa kiuchumi na kufikia TANZANIA ya viwanda
Kwa upande wake diwani Wa kata ya chamwino kwa niaba ya mwenyekiti Wa halmashauri ya wilaya ya chamwino Elias Wilson Kaweya amesema hata katika vitabu vya dini mwanamke ni mshauri mkuu na kuongeza kuwa matokeo ya kaya yanaharibika kama hakuna maelewano kati ya baba na mama nakuwaasa akina mama kujiamini katika mambo mbalimbali ikiwemo katika malezi ya familia ili kuleta maendeleo nchini.
Lakini pia ametoa rai kwa viongozi kuwa karibu na wananchi ili kuleta maendeleo chanya kwa jamii na kuepuka malumbano ambayo hayana tija.