Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 5:02 am

NEWS: WANAUME 4 MBARONI KWA KULA NYAMA ZA BINADAMU AFRIKA KUSINI.

AFRIKA KUSINI: Wanaume wanne wakiwa na umri kati ya miaka 22 na 32 wawili kati yao ni madaktari wa kitamaduni wamefikishwa mahakama ya Estcout kilometa 175 kaskazi magharibi mwa mji wa Durban kwa tuhuma zinazowakabiri za ulaji wa nyama ya binadamu.

Msemaji wa polisi aliimbia BBC baada ya madai hayo mmoja wao alifika katika kituo cha polisi na kusema kuwa amechoka kula nyama ya binadamu.

alipohojiwa zaidi huyo alionyesha sehemu ya mguu na mkono wa binadamu

kisha polisi wakaandamana na mwanaume huyo hadi kwenye nyumba moja iliyo mtaa wa kwazulu -natal ambapo sehemu zaidi za miili ya binadamu zilizatikana .

Msemaji wa polisi aliongeza kuwa uchunguzi bado unaendelea na polisi wameshawashauri watu ambao jamaa zao wametoweka kujitokeza.

Wachunguzi wa visa vya uhalifu wameitwa kutambua sehemu hizo za binadamu, kwa kuwa haijulikana ikiwa sehemu hizo ni za mtu mmoja au watu kadhaa.

Mwezi mmoja uiopita mjini Durban, mwanamume mmoja alikamatwa akiwana na kichwa cha binadamu ambacho inanamiwa alikuwa na mpango wa kikiuza kwa daktari ya kitamadunia.