- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANASAYANSI WAMEFANIKIWA KUMUONDOLEA MTU VIRUSI VYA UKIMWI
Jopo la wanasayansi limetangaza kufanikiwa kumuondolea virusi mwathirika wa Virusi vya Ukimwi ama VVU kwa kutumia tiba ya kumpandikiza uboho kutoka kwa mtu ambaye hajaathirika na virusi hivyo. Huyu ni mgonjwa wa pili Kupewa tiba hiyo.
Hiki ni kisa cha pili kilichoonesha mafanikio kama hayo baada ya kile cha kwanza cha mwaka 2007.
Madaktari wametumia njia ya kupandikiza uboho ili kuviondoa Virusi vya Ukimwi ama VVU kwa mwathirika mmoja wa virusi hivyo vinavyosababishwa UKIMWI. Ingawa wanasifu matokeo ya utafiti huo, lakini wanaonya kwamba ni mapema mno kumthibitishia kwamba amepona.
Mgonjwa huyo, aliiomba timu yake ya matibabu kuficha utambulisho wake.
Matibabu na matokeo yalichapishwa katika jarida la kisanyansi la kimataifa la "Nature" na yanatarajiwa kutangazwa rasmi katika mkutano wa masuala ya tiba utakaofanyika huko Seattle, Marekani siku ya Jumanne.
Kiongozi wa jopo la utafiti huo, Ravindra Gupta, alinukuliwa akisema "Kufikiwa kwa hatua hii kunakoonyesha ahueni kwa mgonjwa huyu wa pili na kulikotokana na mbinu ileile iliyotumiwa awali, kunatokana na mgonjwa wa kwanza wa Berlin kutoonyesha shida yoyote."
Katika visa vyote viwili, wagonjwa walipandikizwa uboho kutoka kwa watu waliokuwa na uwezo wa kuhimili VVU. Lakini pia alisema, kubadilisha chembehai za mwathirika na watu hao kumeonekana kumwezesha mgonjwa kuzuia virusi vya Ukimwi kurejea baada ya matibabu.