Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 10:22 am

NEWS: WANAOPATA AJALI ZA BODABODA WAOGOPA KUSEMA UKWELI KUHOFIA KUKATWA MIGUU

DODOMA: IMEELEZWA kuwa watu wanaopata ajali za pikipiki (bodaboda) wanashindwa kueleza ukweli kwamba wamepata ajali za usafiri huo pindi wapopelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma kwa ajili ya matibabu kwa kuhofia kukatwa miguu.

Kutokana na taarifa hiyo ambayo inadaiwa ya uzushi imepelekea hospitali hiyo kushindwa kupata takwimu za ajali za pikipiki kwani hakuna mgonjwa anayefika hospitalini hapo akiwa aimepata ajali na kueleza kuwa amepata ajali ya pikipiki kwa kuhofia kukatwa miguu.

Hata hivyo inaelezwa kuwa wapo wachache ambao wanauwezo wa kusema kuwa alipata ajali ya pikipiki na hii anajitoleza baada ya kupatiwa matibabu kwa mara kwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma Kamimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dk.ERNEST IBENZI alisema hali hiyo inasababosha hospitali hio kutokuwa na takwimu za majeruhi ambapo hapa anaeleza idadi ya majeruhi wanaopokelewa kwa siku katika hopitali hiyo kutokana na ajali mbalimbali.

Licha ya hospitali ya Rufaa Makoa wa Dodoma kukosa takwimu za ajali za pikipiki lakini hapa Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Dodoma Marison Mwakyoma akabainisha takwimu hizo.

Kutokana na ajali hizo kuelezwa kupungua hapa anaeleza jitihada ambazo zimetumika ili kuhakikisha ajali hizo zinapunguzwa ikilinganishwa na kipindi cha mwaka jana.

Aidha watumiaji wa bodabodo wanakumbushwa kutii sheria bila shuruti ikiwa ni pamoja na kuvaa kofia ngumu huku ikielezwa kuwa kupigwa marufuku matumizi ya pombe aina ya viroba imekuwa chanzo cha kupunguza ajali katika Mkoa wa Dodoma.