Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 10:39 pm

NEWS: WANAOJIPENDEKEZA KWA JPM WAONYWA

DODOMA: ASKOFU mkuu wa Kanisa la Endtime Haverst Tanzania, lenye makao yake makuu Dodoma Dk.Elia Mauza amewashukia baadhi ya viongozi wa Dini mbalimbali kuwa Hawamsaidii Rais Dk.John Magufuli kwa kumueleza ukweli wa mambo yanayoendelea hapa nchini na badala yake wanajikomba kwake.

Askofu Dk .Mauza alitoa kauli hiyo jana katika ibada maalumu ya kutangaza kuliombea taifa na kutoa elimu kwa wananchi juu ya rasilimali zao na uchumi uliopotea kurejeshwa wa watanzania wote.

Katika ibada hiyo askofu Dk. Mauza alisema pamoja na juhudi mbalimbali za Rais Magufuli lakini bado kuna majipu na vijipu uchumgu ambavyo bado hajaweza kuvitambua na kuvitumbua kutoka na viongozi wa dini kujikomba kwake na kushindwa kumweleza ukweli rais.

Akizungumzia kitendo cha rais kuvunja iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) Dk.Mauza alisema bado Rais Magufuli ana kazi ya kufanya kwani ni lazima walioporwa ardhi na iliyokuwa CDA ni lazima warejeshewe viwanja vyao na kupewa fidia kwa wale ambao wanastaili kulipwa fidia.

Pia alisema wale waliokuwa wakifanya kazi CDA walirudishwe katika vitengo hivyo licha ya kuwa CDA imehamishiwa Manspaa kwa madai kuwa watumishi hao waliokuwa CDA ndo waliosababisha wananchi wa Dodoma kuishi kama wakimbizi katika nchi yao.

Akitolea mfano katika eneo la Mbuyuni katika kata ya Kizota Manispaa ya Dodoma ambapo iliyokuwa CDA ilisema kuwa eneo la Mbuyuni ni sehemu ya Viwanda huku wakimpatia mwekezaji wa machinjio ya nyama na wangine kijimilikisha viwanja na kusababisha kuwepo kwa mtafaruku mkubwa na kusababisha wananchi kuichukia serikali yao.

“Mimi nikiwa kiongozi wa Kiroho ambaye nipo makao makuu ya nchi nakutaka rais Magufuli kuhakikisha unatumbua hivi jipu uchungu ambavyo bado vipo wakazi wa Dodoma bado wanahofu hawajui hatima ya maisha yao kwani wapo ambao tayari walisha porwa maeneo yao.

“Wapo wale ambao walikuwa wakipambana ili walipwe fidia zao lakini cha kusikitisha ni pale wale waliokuwa wafanyakazi wa CDA kurudishwa katika vitengo vile vile licha ya kuwa CDA imevunjwa hivyo basi chonde chonde Rais Magufuli ingilia kati haraka vinginevyo patakuwa hapatoshi”alissisitiza Dk. Mauza.

Katika hatua nyingine Askofu Dk. Mauza aliwataka viongozi wa Kiroho nchini kuachana na tabia ya unafiki na kujipendekeza kwa Rais badala yake wanatakiwa kumsaidia kumwambia ukweli kuhusu nchi inavyoelekea.

“Unajua watumishi wa Mungu tupo wengi lakini waliowengi ni wanafiki na wanajipendekeza kwa rais kwa sababu tu ya bahasa ambazo wanajuwa labda kwa baadaye atatumwa dereva kuleta bahasha, mimi siyo wa hivyo.

“Wanaofanya ufisadi tunao makanisani misikitini na yapo mambo mengine ambayo tunayaona lakini rais hayaoni ni lazima tumwambie ukweli mimi najua bahasha yangu tayari ipo mbinguni bhasha nitaipata tu hivyo rais Magufuli lazima uweze kujua kuwa Dodoma ni lazima kuangaliwe kwa jicho la kuwa makao makuu kwa kuhakikisha migogoro ya ardhi inakwesha na watu wanapata haki zao kwa wakati” alisema.

Kuombea taifa.

Kwa upande mwingine Dk. Mauza ametangaza kuwepo kwa kongamano la siku 5 za kuliombea taifa pamoja na kuiombea nchi ya Israel.

Alisema kongamano hilo licha kuziombea nchi hizo lwa lengo la kumwombea Rais Dk. John Magufuli pamoja na rais wa Israel,Benjamini Tenyau, bado kutakuwepo na semina ya kuwafundisha wananchi kurudia kwa uchumi wao uliopotea.

Uchaguzi

Katika hatua nyingine kanisa hilo limefanya uchaguzi wa kikatiba na kumpata askofu mkuu Dk.Askofu Mkuu Elia Mauza ambaye ataongoza kanisa hilo kwa miaka 20,Mwanasheria Mkuu,Katibu Mkuu, Mtunza fedha,Mkurugenzi wa Uinjilisti na Umisheni,Mkurugenzi wa Vijana na Mkurugenzi wa Watoto.

Uchaguzi huo ulienda sambamba na kufanya marekebisho ya katiba ya kanisa la Endtime Haverst Tanzania kwa lengo la kuimarisha kanisa hilo.