- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA RASIMALI KUFANYA KAZI KWA KUJITOLEA.
DODOMA:Mkurugenzi Wa Maendeleo Ya Jamii Patrick Golwike Amewataka Wananchi Kutumia Rasilimali Walizonazo Kufanya Kazi Kwa Kujitolea.
Bw. Golwike ameyasema hayo katika Zoezi La Kuamsha Ari Za Wananchi kushiriki kazi za maendeleo lililofanyika leo katika Shule ya sekondari ya kata ya Iyumbu Jijini Dodoma.
Amesema jamii imekuwa na mwamko mdogo katika kushiriki kazi mbalimbali za mendeleo hivyo zoezi hilo lilaleta taswira kuwa wao kama wataalamu hawako kwa ajili ya kutoa mikopo hata kuwajibika kwa kushirikiana na jamii ili kuweza kujiletea maendeleo.
Pia ameendelea kusisitiza kuwa Sera ya Maendeleo ya jamii inasisitiza kujenga jamii inayojitegemea,inayoongeza kipato na Taifa linalojitegemea.
Licha ya hayo amesema zoezi hilo limeokoa sh milion 6.5 za ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara vya shule ya sekondari hiyo ,baada ya kushiriki ujenzi wa kumwaga jamvi katika vyumba hivyo.
Pia amewataka maafisa Maendeleo kutambua wajibu wao ili kuhakikisha miradi ya maemdeleo inafanyika kikamilifu.
"Moja ya kazi za Maafisa Maendeleo ni pamoja kusimamia miradi hivyo ni lazima tuamshe ari kwa wananchi kushiriki katika miradi ya maendeleo," alisema Golwike.
Mbali na hayo Wananchi Wa Kata Ya Iyumbu akiwemo Janet Daud Moses Leonard Wamesema Kufuatia Shule Ya Sekondari Ya Kata Yao Kutosajiliwa Kutokana Na Kutokuwepo Kwa Maabara Na Vyoo Vya Kudumu Wamelazimika Kutumia Nguvu Kazi Ya Pamoja Kuanza Ujenzi Wa Maabara Tatu na kudai kuwa Kukosekana inawalazimisha watoto wao Kwenda Kusoma Shule Jirani
Hivyo wamesema Kukamilika Kwa Maabara Hiyo Itawezesha Shule Hiyo Kusajiliwa Na Hatimaye Wanafunzi Kuacha Kutembea umbali mrefu wa kilomenta 12
Akitoa taarifa ya ujenzi wa vyumba hivyo vya maabara Afisa mtendaji wa Kata ya Iyumbu Vicent Leo Amesema Ujenzi Wa Maabara Hiyo Ulianza Mwezi December Mwaka 2018 Ambapo Amesema Wananchi Wamekuwa Wakijitolea Kwa Shughuli Huku Akibainisha Kuwa Kwa Sasa Wanaendelea Kuchangishana Ili Kumalizia Hatua Za Mwisho Zilizobaki.
Amesema ujenzi wa shule hiyo utasaidia kupunguza adha ya wanafunzi kutembea kilomita 24 kwa ajili ya kwenda shule ya sekondari Kisasa wakitokea eneo la Iyumbu.
Amesema wanaamini pamoja na nguvu kazi ya wananchi wa eneo hilo na wadau mbalimbali wanaojitokeza nyumba hivyo hadi kufikia mwakani vitakuwa vimekamilika.
Naye Afisa Tarafa wa Wilaya Dodoma Neema Nyalege ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi amewapongeza maafisa maendeleo kutokana na jitihada walioonyesha katika kuchangia Maendeleo kwenye ujenzi huo.
Amesema vyumba vya maabara katika sekondari ni muhimu hivyo ni vema wananchi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuamka kufanya shughuli za maendeleo hususani za ujenzi wa vyumba vya maabara ambavyo ni muhimu kwa wanafunzi kufanya kazi kwa vitendo.
Zoezi hili lilishirikisha Wadau Mbalimbali Wakiwemo Watumishi Kutoka Wizara Ya Afya Maendeleo Ya Jamii Jinsia Wazee Na Watoto na Baadhi Ya Wakazi Wa Kata hiyoi pia wametoa mifuko ya Saruji 120 ambayo imegaharimu zaidi ya milioni mbili.