Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 7:47 pm

NEWS: WANANCHI WATAHADHARISHWA MATAPELI

DODOMA: UONGOZI wa Kanda ya Kati umewatahadharisha wananchi kutothubutu kuwasiliana na viongozi wa iliyokuwa Taasisi ya kusimamia maonyesho ya wakulima Nane Nane(TASO) kwa lengo la kupatiwa viwanja katika maonyesho hayo kwani Taasisi hiyo imekwisha futwa.


Akizungumza na waandishi wa habari hii leo kwa niaba ya wakuu wa Mikoa ya Dodoma na Singida,Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mh.Simon Odunga amesema wananchi wanatakiwa kuwa makini kwani kumekuwa na baadhi ya viongozi wanaowatapeli wananchi kwa kuwauzia viwanja ili hali (TASO) ilikwisha pigwa marufuku kujihusiha na shughuli za uratibu wa maonyesho hayo


Aidha akitoa agizo la Serikali Odunga amewataka viongozi wa TASO kukabidhi mali zote kwa uongozi wa Mkoa na endapo wataendelea kukaidi agizo hilo watachukuliwa hatua za kisheria.


Hata hivyo pia amewasihi wananchi kutumia fursa hiyo kuhudhuria kwa wingi katika maonyesho hayo kwa ajili ya kufanya biashara na kujifunza kutokana na shughuli mbalimbali zitakazokuwa zikiendelea

Maonyesho ya Nane Nane kanda ya Kati yanaanza Agost mosi ambapo yatafunguliwa rasmi Agost 03 na Spika wa Bunge Mh.Job Ndugai na kufungwa Agost 08 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh.George Simbachawene ambapo pia yamebeba kauli mbiu isemayo zalisha kwa tija mazao na bidhaa za kilimo mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati