Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:22 am

NEWS: WANANCHI WAMZOMEA MBUNGE WAO

Mwanza.:Wakazi wa Ilemela mkoani Mwanza walimkana na kuzusha vurugu kwa mbunge wao, Angelina Mabula mbele ya waziri Lukuvi na Mawaziri wengine saba wanaozunguka nchi nzima kupokea kero za migogoro ya ardhi na kupendekeza nini kifanyike ili kuimaliza tatizo hilo la muda mrefu.

Wakazi hao walimzomea mbunge huyo baada ya waziri wa ardhi, William Lukuvi kumtaka awasalimie na kuongea chochote kwa wapiga kura wake.

Lakini Kabla ya Lukuvi kumalizia kauli yake ilisikika miguno ya wakazi hao wakisema hakuna, hakuna, hakuna, hatumtaki, hapana.

Hali hiyo ilimshtua Waziri Lukuvi aliyelazimika kuwatuliza wananchi hao na baadae mbunge huyo alizungumza kwa tabu licha kukataliwa.

Angelina Mabula ni Naibu waziri wa Ardhi na nimbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na miongoni mwa mawaziri nane wanazunguka katika ziara yao hiyo kutatua migogoro ya Ardhi.