- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANANCHI WAHOJI KUBEBWA KWA BAADHI YA VIONGOZI WA UMMA.
Dodoma: Baadhi ya wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Itigi Mkoani Singida wameonyeshwa kusikitishwa na hatua ya rais John Magufuli kuwafuta kazi baadhi ya watumishi wa Umma kutokana na zoezi la uhakiki wa vyeti ambao walibainika kugushi na wengine kutumia vyeti zaidi ya mmoja.
Hayo yameelezwa leo Wilayani Itigi na wakazi hao wakati wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti kuhusiana na hatua hiyo ya rais.kuwafuta kazi wafanyakazi hewa.
Malalamiko hayo ya wananchi hao yamekuja kufuatia zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma uliofanyika kuanzia mwezi machi mwaka jana na hivyo kumkumba Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Mji huo kuwa na cheti feki.
Aidha kwa upande wake Katibu wa Dayosisi ya Rift Valley Mchungaji Daudi Manase amesema kuwa amesikitishwa na kitendo hicho cha Waziri Kairuki kutoa kauli ambao imeonyesha dhahiri kuwabeba baadhi ya viongo wa umma ambao ni wanasiasa ni wanasiasa na kwamba zoezi hilo la uhakiki haliwahusu wanasiasa kwani sifa yao ni kujua kusoma na kuandika.
Akithibitisha taarifa kuhusu Kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Itigi ,Zuberi Abdalla kutumia vyeti ambayo si vyake,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi SHIJA LUHENDE amesema zoezi litasaidia kuharakisha maendeleo.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John magufuli alikabidhiwa ripoti ya uhakikiwa vyeti na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala bora,Angelah Kairuki na kubaini kuwepo kwa watumishi waliofoji vyeti wapatao 9,932 huku watumishi wengine 3076 wakitumia cheti kimoja zaidi ya watu wawili.