Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 7:41 pm

NEWS: WANANCHI WA KIGOMA KUFAIDIKA NA MRADI WENYE THAMANI YA SH. BILIONI 110

Kigoma: Umoja wa mataifa unatarajiwa kuzindua mradi mkubwa wa maendeleo Mkoani wa Kigoma wenye thamani ya Shilingi 110 bilioni. Mradi ni wa miaka minne na utahusisha sekta mbali mbali ikiwemo Nishati, ajira Kwa vijana na wanawake, kilimo, maji nk. mpaka sasa mradi umesha tumia zaidi ya Bilioni 26, kabla ya uzinduzi wa programu hiyo.

Nae mbunge wa kigoma ujiji Zitto kabwe amefurahishwa na kushukuru uwekezaji huo kwani unaleta tija kwenye maendeleo ya mkoa huo na Tanzania kwa ujumla wake " Nawashukuru UN Kwa kuitikia wito wetu wa kuisaidia Kigoma kufuatia mkoa wetu kutunza wakimbizi wengi sana. Sisi Wabunge wa Kigoma tutasimamia kuhakikisha miradi hii inakuwa na mafanikio makubwa Kwa wananchi wetu"


Ingawa mradi huo ulianza tangu July 1, 2017 lakini unatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu mradi huu utachukua muda wa takribani miaka 4 ambayo bajeti yake ni zaid ya Dola za kimarekani 55milioni.