Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 11:28 pm

NEWS: WANANCHI UINGEREZA WAPINGA KUSIMAMISHWA KWA SHUGHULI ZA BUNGE

Maalfu ya wananchi nchini Uingereza kote wanatarajiwa kushiriki kwenye maandamano ya kupinga kusimamishwa kwa shughuli za Bunge nchini Humo.

Maandamano hayo yameitishwa na wapinzani wa Brexit wa kundi linaloitwa "Another Europe is Possible" yaani Ulaya nyingine yawezekana. Malkia Elizabeth wa pili ameridhia hatua ya Waziri Mkuu Boris Johnson ya kulisimamisha bunge hadi katikati ya mwezi Oktoba ambapo zitabakia takriban wiki mbili ambapo Uingereza itapaswa kujiondoa umoja wa Ulaya.

Tokeo la picha la Demostration in england tommor

Wachambuzi wanasema ni hila ya serikali kuwanyima wabunge uwezekano wa kuzuia Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya bila ya mkataba.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anakabiliwa na changamoto za kisheria kutokana na hatua yake ya kusimamisha bunge mnamo siku ya Ijumaa. Johnson ametahadharisha juu ya hatua za kuuvuruga mpango wa Uingereza wa kutafuta makubaliano sahihi na Umoja wa Ulaya.

Amesema kadiri washirika na marafiki wa Uingereza wanavyozidi kufikiria kwamba mpango wa Brexit unaweza kusimamishwa na nchi hiyo inaweza kuendelea kuwamo kwenye Umoja huo ndivyo matatizo yanavyozidim kujitokeza na kusababisha uwezekano mdogo wa kufikiwa makubaliano yanayohitajiwa na Uingereza.

Waziri Mkuu wa Uingereza amsema nchi yake kushindwa kuondoka kutoka kwenye Jumuiya ya Ulaya kama walivyochagua wapiga kura kwenye kura ya maoni kutasababisha athari kubwa kwa vyama vikubwa vya kisiasa nchini Uingereza.

Mapema Ijumaa, mahakama ya Scottland ilikataa ombi la kuzuia maamuzi ya bwana Johnson ya kusimamisha bunge, lakini imeamuru usikilizwaji kamili juu ya suala hilo ufanyike katika siku tatu zijazo.