- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: "WANANCHI JIANDAENI NA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2019", DC MPOGOLO.
SINGIDA: Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo amewahimiza wananchi kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 kwa kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kupiga kura siku ikifika.
Hamasa hiyo anaitoa zikiwa zimesalia siku chache kuelekea siku ya kupiga kura novemba 24 mwaka huu.
Akizungumza septemba 20 katika mkutano wa hadhara wa mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu wilayani humo,Mpogolo amesema mwaka 2014 katika uchaguzi uliopita akina mama wengi walijitokeza kujiandikisha lakini hawakupiga kura jambo ambalo halipaswi kutokea kwa sasa.
Amesema mwaka huo akina mama elfu 46 walijiandikisha katika daftari la wapiga kura,lakini waliopiga kura ni elfu 23 tu.
“Ili mumpende Rais Magufuli ni lazima mjitokeze kupiga kura na mumchague mtu anayeendana nae ili kuweza kuunga cheni,ukiwa na cheni ina vipande vingine vya mbao vingine vya chuma lazima upande fulani maendeleo hayatokwenda vizuri,sasa mmepata jembe mchapakazi Mtaturu ungeni cheni hiyo ili maendeleo yaweze kuja,”.alisema Mpogolo.
Amewataka akina mama hao kutoogopa kutishwa na mtu yoyote bali washiriki vizuri katika uchaguzi huo kwani ulinzi na usalama umeimarishwa maeneo yote.
Kwa upande wake Mtaturu amesema vyama vya upinzani ni kama watoto anapokuja mgeni anasubiri mgeni achukue paja ndio nayeye apate.
“ CCM ni Chama kikongwe ,kina heshima na kinatafsiri vitendo matatizo ya watu,kina umoja,upendo na mshikamano na amani tuliyonayo,CCM ni chama kubwa kimekaa muda mrefu lakini hakijachoka kuwaongoza watanzania,”alisema Mtaturu.
Amewataka wananchi muda ukifika wachague njia iliyonyooka kwak uchagua CCM.