- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANAJESHI 53 WAUWAWA SHAMBULIO LA KIGAIDI MALI
Takribani Wanajeshi hamsini na watatu wameuawa jana Ijumaa katika "shambulio la kigaidi" kwenye kambi ya jeshi la Mali kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, serikali ya nchi hiyo imesema.
Shambulio hilo ni moja ya shambulizi baya kabisa dhidi ya jeshi la Mali katika ghasia za wanamgambo wa kiislam za hivi karibuni.
Raia mmoja pia aliuawa katika kambi ya nje ya Indelimane, katika mkoa wa Menaka, karibu na mpaka na Niger, waziri wa mawasiliano wa nchi hiyo Yaya Sangare amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Aidha waziri huyo ameongeza kuwa kwa sasa hali imedhibitiwa,Utafutaji na mchakato wa kutambua miili unaendelea,na kwamba manusura 10 walipatikana katika kambi ya nje ambayo imeshuhudia uharibifu mkubwa..