- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANAFUZI WANAOSOMEA URUBANI KIPEWA MIKOPO NCHINI
Dar es Salaam. Serekali kupitia kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema yupo katika hatua za mwisho ya mazungumzo na Wizara ya Elimu ili itoe mikopo kwa wataalamu wanaosomea sekta ya anga hasa marubani.
Kamwelwe ameeleza hayo leo, Jumatatu Juni 24, 2019 wakati akifungua kongamano la pili la wadau wa sekta ya anga lililoandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Kongamano hilo, lina lenga la kujadili mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta hiyo na mbalimbali zitawasilishwa ikiwemo mchango wa sekta ya anga kwenye ajenda ya kuipeleka Tanzania ya viwanda.
Kamwelwe ambaye pia mbunge wa Katavi (CCM) amesema tayari ameshazungumza na viongozi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) katika kufanikisha mchakato huo ili bodi hiyo ishiriki kikamilifu kuwasaidia wataalamu hao.
“Kulikuwa na hoja ya kwamba wataalamu hawa wanahitaji fedha nyingi, lakini nikawaambia hawa watalipa haraka kuliko hao wengine wanaokopeshwa. Nimeangalia vizuri hii fani rubani kufundishwa hadi kuiva ni fedha nyingi.”