Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 9:16 pm

NEWS: WANAFUNZI WALIOCHORA PICHA YA RAIS WA BURUNDI WAACHIWA HURU

Serekali nchini Burundi imewaachilia huru wanafunzi watatu wa kike ambao walikamatwa wakishutumiwa kuichafua kwa kuichorachora picha ya rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kwenye vitabu vyao vya shule. hii ni kwa mujibu wa Waziri wa sheria wa nchi hiyo Bw. Aimée Laurentine Kanyana

Pierre Nkurunziza

Kushikiliwa kwa wasichana hao takribani majuma mawili yaliyopita kwa shutuma za kumtusi rais kulizusha kampeni mitandaoni za kutaka wasichana hao waachiliwe kampeni iliyokua na jina #FreeOurGirls, watu wakituma picha kwenye mitandao ya Twitter.

Waziri amesema wasichana hao wenye miaka 15,16 na 17 wameachiwa huru kwa muda.

''Tunawataka wazazi kuboreha elimu ya watoto wao .Tunawakubusha watoto kuwa wanapaswa kuheshimu mamlaka,na kuwa umri wa kuwajibishwa ni miaka 15

Walikamatwa walipokuwa katika shule ya ECOFO iliyopo katika mkoa wa kaskazini wa Burundi wa Kirundo tarehe 12 mwezi Machi ,2019

Awali walishitakiwa wakiwa wanafunzi saba, lakini wanne wakaachiliwa huru.

mchoro