- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANAFUNZI WA MSALATO GIRLS WATEMA POVU KWA JAFO WAAHIDI KUINGIA 10 BORA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA
DODOMA: Wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wasichana ya Msalato Manispaa ya Dodoma wamemuahidi Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Mhe. Selemani Jafo kwamba watapambana ili katika matokeo ya kidato cha sita mwakani shule yao iwe miongoni mwa shule kumi bora nchini.
Ahadi hiyo ilitolewa na wanafunzi hao katika ziara ya Naibu Waziri Jafo alipotembelea shule hiyo kukagua ujenzi wa miundombinu inayojengwa na serikali ili kuirudisha shule hiyo katika hadhi yake.
Shule hiyo ni miongoni mwa shule kongwe 88 zilizo katika mpango wa ukarabatiwa na serikali ambapo ndani ya miaka 4 shule hizo zitakuwa ni shule zenye ubora wa hali ya juu kwa kuboreshewa mazingira yake yakiwemo mabweni, madarasa, vyoo, mabwalo, mifumo ya maji na umeme, pamoja na nyumba za walimu.
Katika shule hiyo, serikali hadi sasa imeshakamilisha ukarabati wa mabweni nane, mfumo wa umeme na maji.
Aidha Serikali imejipanga kuendelea na ukarabati wa madarasa na ujenzi wa madarasa mengine manne mapya, ukarabati wa bwalo la chakula, majengo ya utawala, na nyumba za walimu.
Kufuatia uboreshaji huo, Wanafunzi wameishukuru serikali na wamemuahidi Naibu Waziri huyo kwamba watahakikisha wanajitahidi ili mwakani shule yao iwe miongoni mwa shule kumi bora katika matokeo ya kidato cha sita.
Akizungumza na wanafunzi hao, Naibu Waziri Jafo amewahakikishi watanzania kwamba mpango wa serikali ni kuboresha shule za umma ili ziweze kutoa elimu bora hapa nchini.
Mwaka jana, Naibu Waziri Jafo alitembelea shule hiyo na kuwataka wanafunzi wa kidato cha sita kuhakikisha wanafanya vizuri katika mitihani yao ili shule hiyo itoke kutoka shule ya 21 katika matokeo ya kidato cha sita mwaka jana ili waingie 10 bora. Jambo ambalo katika matokeo ya mwaka huu shule hiyo imeshika nafasi ya namba 14 kitaifa.