- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANAFUNZI CHUO ST. JOSEPH WAMETULETEA ATM YA KUTOA PEDI ZA KIKE
Wanafunzi wanne kutoka chuo cha Mtakatifu Joseph cha jijini Dar es salaam wamebuni mashine ya ATM ambayo itakayokuwa ikitoa taulo za kike(pedi) au pedi za kina dada kwa bei nafuu zaidi.
ATM hii inatumia sarafu au kadi maalum ambayo hujazwa fedha na kukabidhiwa mwanafunzi.
Mashine hii inatarajiwa kufungwa vyoo vya shule, ofisini, kwenye masoko ama kwenye saluni za kike, na ili kuitambua mahali ilipo inatumia App maalum katika simu.
Msemwa anasema mwanafunzi ata "atapitisha" kadi kwenye mashine na kukatwa shilingi 2,000 ama 2,500 kulingana na aina ya pedi iliyowekwa kwenye mashine, na kadi ikiisha fedha anaweza kutumia sarafu ya shilingi 500 na kuitumbukiza kwenye sehemu maalum ya mashine hii akaweza kupata pedi kwa mtindo wa dharula.
Wabunifu wa Mashine hii wametumia miezi minne kuja na ubunifu huu, ingawa haujakamilika asilimia mia moja, hatua iliyofikia ni ya kuboresha kitaalam zaidi.
Mkuu wa Kitengo cha ubunifu kutoka Chuo cha Mtakatifu Joseph, Dk Lawrence Kerefu anasema, kwa sasa mashine hiyo na vitu vingine vilivyobuniwa na wanafunzi wa chuo hicho, wameviwekea mkakati wa kuviboresha zaidi kabla ya kuanza kutumika.