- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANAFUNZI 7 WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA UKUTA
Wanafunzi saba wa Shule ya msingi katika mtaa wa Dagoretti jijini Nairobi nchini Kenya, wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta na paa la darasa lao la orofa moja Jumatatu asubuhi.
Mkasa huo ulitokea wakati wanafunzi hao walipokuwa wameingia darasani wakisubiri kuanzia masomo yao katika Shule hiyo binafsi inayoitwa Precious Talent.
Msemaji wa serikali Cyrus Oguna amesema wanafunzi 57 wamelazwa katika Hospitali Kuu ya Kenyatta wanakoendelea kupata matibabu.
“Hadi sasa, tunathibitisha kuwa wanafunzi saba wamepoteza maisha na wengine 57 kujeruhiwa na wanaendelea kupata matibabu,” amesema.
Mamia ya wakaazi wa mtaa huo na wazazi waliokuwa wa kwanza kufika katika eneo hilo la mkasa walionekana wenye hasira kwa kile walichokisema, maafisa wa serikali ya Kaunti ya Nairobi walichukua muda mrefu kufika katika Shule hiyo kuwaokoa wanafunzi hao.
Imebainika kuwa, ujenzi wa Shule hiyo hakuwa imara kwa sababu zilijengwa kwa vifaa duni vya ujenzi, yakiwemo mabati na mbao.
Shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 800, kutoka mtaa huo wenye watu wanaoishi katika maisha magumu.