- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAMACHINGA WAANZA KUTIMULIWA DAR
Dar es salaam: Manispaa ya wilaya ya Kinondoni jana imewatimua wamachinga wote waliopo kandokando ya barabara ya mabasi yaendayo kasi Katika barabara ya Morocco. Operesheni hiyo iliyoanza kwenye majira ya saa 11 mpaka saa moja jioni katika eneo la kinondoni studio, Jiji Dar es salaam.
Akizungumza na Muakilishi.com Jana Afisa Masoko wa manispaa ya kinondoni Bw. Zahoro Haruna amesema kuwa wanataka wamachinga wote wanao fanya biashara kando kando ya barabara waondoke mara moja kwa sababu tayari wamesha watengea maeneo maalumu ya kufanya biashara hizo kinyume na hapo watakuwa wanavunja sheria.
Aidha kwa upande wa wamachinga wenyewe wanadai kuwa wao wameruhusiwa kufanya biashara hizo kwa amri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kauli ambayo kwa mujibu wa afisa masoko wa manispaa ya kinondoni amesema kuwa wananchi wametafsiri vibaya kauli ya Mh Rais Magufuli na kusema kuwa Rais alisema tuwatafutie maeneo ya kufanyia biashara kitu ambacho sisi tumesha fanya.
Haruna amesema kuwa kwa wale wenye mali zao wafike katika ofisi ya wilaya ya Kinondoni kwa utaratibu zaidi wa kisheria