Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 5:30 pm

NEWS: WALIOSHIKWA NA SHEHENA YA ALIMASI AIRPORT WABURUZWA MAHAKAMANI LEO

Dar es salaam: Watu waliokamatwa na vifurushi vya almasi yenye thamani ya Sh 32.2 bilioni katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere(JNIA), wamefikishwa mahakamani Kisutu asubuhi ya leo siku ya Ijumaa kujibu mashataka yao.

Watuhumiwa hao walikamatwa na mzigo huo Septemba 9 mwaka huu ambao ulizuliwa na Serikali ili ufanyiwe tathimini upya kujua thamani halisi baada ya thamani iliyotumika kutiliwa mashaka na Serikali. Almasi hiyo ilikuwa inathamani ya dola za kimarekani 29 Milioni
Jeshi la polisi liliwashikilia watuhumiwa wanne kwa uchunguzi na hatua nyingine za kisheria baada ya kuzuia mzigo huo.

Mzigo huo wa almasi ulikuwa unatoka mgodi wa Mwadui ambao ni wa ubia kati ya Serikali na kampuni ya Petra Diamonds ya Afrika Kusini kwa hisa 25 za Serikali na Petra Diamonds hisa 75.

Agizo la kuitaifisha almasi hiyo ilitolewa na Waziri wa Fedha na MipangoMhe.Dkt. PhilipIsdorMpango(Mb), mara baada ya kupokea ripoti ya usafirishwajiwa madini hayo, pamoja na kuukagua mzigo huo. Dkt. Mpango alisema endapo mzigo huo ungesafirishwa kwenda nje ya nchi,nchini Ubelgiji na Kampuni ya madini ya Williamson Diamond Ltd,Taifalingeingia hasara ya mabilioni ya fedha kwani palikuwa na udanganyifumkubwa katika ukokotozi wa hesabu zake, hasa gharama yake pamoja nagawio halisi la serikali