- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WALIOMFUNGULIA MAKONDA HABARI ZAKE, WAPEWA ONYO KALI
Dar es salaam: Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) kupitia Mwenyekiti Maalum wake, Walace Mauggo ameeleza kuwa jukwaa kwa kauli moja limetoa onyo kwa viongozi wake kutorudia yale ambayo waliyoyafanya.
“Baada ya kutafakari na kutathmini mwenendo wa mkutano huo, jukwaa lilobaini kuwepo kwa kasoro kubwa wakati wa kurejesha mahusiano wa kikazi na kiongozi ambaye habari zake zilizuiwa kuripotiwa kwa takribani miezi mitano,” alieleza Bw.Mauggo.
Hii imekuja Kufuatia maoni ya baadhii ya watu mbalimbali na waandishi wa habari kutoridhika na maamuzi ya Jukwaa la Wahariri (TEF), kupitia Nevi Meena na Balile kufanya mkuta na waandishi wa habari bila kushirikisha uwongozi wa juu na kuingilia maamuzi ya uwongozi wa juu.
Baada ya onyo hiyo Pia wametakiwa kuhakikisha kunapotokea masuala makubwa kama hayo ambayo yashafanyiwa maamuzi na mkutano mkuu na taasisi nyingine za habari yanarudiswa maamuzi kwa wanachama kabla ya hatua za mwisho.
Mauggo ameeleza kuwa TEF haitasita kuchukua hatua kwa kiongozi au mtu yoyote atakayeonekana kutishia usalama wa wanahabari, uhuru wa uhariri na vyombo vya habari.