- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : WALIOFARIKI KWA GONGO WAFIKIA 10
Dar es Salaam. Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imesema idadi ya watu waliofariki dunia kwa kunywa kinywaji kinachosadikiwa kuwa gongo imefikia 10.
Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema leo Alhamisi kuwa wananchi walitoa taarifa baada ya hali za waliotumia pombe hiyo eneo la Kimara kubadilika.
Amewataja waliofariki dunia kuwa ni Mohamed Issa (67), Kabugi Rashid (64), Stanslaus Joseph (58), Stephen Isaya (61), Monika Rugaillukamu (42), Alex Madega (41), Hamis Mbala (35) na Ekson Nyoni (28).
Wengine ni mwanamke aliyekuwa akiuza pombe hiyo aliyefahamika kwa jina moja la Anoza na Maleo Ramadhan (45) mkazi wa Kimara Stop Over.
Kamanda Mambosasa amesema katika upelelezi wa awali wamebaini chupa tatu za ujazo wa lita moja zikiwa zimejazwa pombe inayodhaniwa kuwa ni gongo.
"Vielelezo vyote vya tukio hili vimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini chanzo halisi cha vifo hivyo," amesema.
Amesema upelelezi unaendelea kubaini wote waliohusika katika tukio hilo, akiwataka wananchi kuacha kunywa na kula vitu visivyo na ubora wala kuhakikiwa na mamlaka husika.