- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WALIOFARIKI AJALLI YA MOROGORO WAONGEZEKA, WAFIKIA WATU 100
Idadi ya watu waliofariki kutokana na mlipuko wa lori la mafuta Agosti 10,2019 katika eneo la Msamnvu mjini Morogoro kwasasa imefikia watu 100.
Idadi hiyo imefikia kiwango hicho kutokana na majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuendelea kuaga dunia siku hadi siku.
wakati wa ajali hiyo Watu 62 walithibitishwa kufariki na zaidi ya 70 kujeruhiwa, na toka hapo idadi ya vifo imekuwa ikiongezeka taratibu.
Awali idadi ya majeruhi 46 walisafirishwa kutoka Morogoro mpaka Muhimbili kwa matibabu ya kibobezi, lakini mpaka asubuhi ya leo, Jumatano Agosti 21 ni majeruhi 15 tu ndio waliobaki Muhimbili.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari wa Muhimbili, Bw Amini Aligaesha kati ya majeruhi 13 wamelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na wawili wapo kwenye wadi ya wagonjwa wa kawaida.
Wengi wa majeruhi waliokimbizwa Muhimbili walikuwa wameunguzwa na moto kwa asilimia 80 na kuendelea.
Mkasa huo ulitokea majira ya saa mbili asubuhi ya Jumamosi baada ya lori lilibeba shehena ya petroli kuanguka katika mji wa Morogoro, na watu kuanza kuchota mafuta yaliyomwagika kisha mlipuko mkubwa kutokea.
Kumekuwa na hisia tofauti juu ya ajali hiyo lakini Rais wa nchi hiyo John Magufuli amewataka wananchi wake kuacha kuhukumu waliofariki na majeruhi.