- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WALIOCHOMA KITUO CHA POLISI BUNJU A WAHUKUMIWA MAISHA JELA
Dar es salaam: Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jiji Dar es salaam leo Februari 22, 2019 imewahukumu kifungo cha maisha jela Washtakiwa nane akiwemo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bunju A, jijini Dar es Salaam, Yusuph Salehe baada ya kukutwa na hatia ya kuchoma kituo cha Polisi kilichopo Bunju A. Jijini hapa.
Katika kesi hiyo, Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu imewaachia huru washtakiwa wengine tisa baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao.
Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba huku akitamka kuwa kifungu cha 319 A cha Sheria ya Kanuni ya adhabu kinatamka kuwa washtakiwa wanaokutwa na hatiani adhabu ni mpaka kifungo cha maisha jela.
Muakilishi ilipiga stori na Ndugu wa mwenyekiti huyo akionesha kutilia shaka hukumu hiyo na wanajipanga kukata rufaa dhidi ya maamuzi hayo "hiyo sheria anayosema hakimu hukumu hiyo ni adhabu ya mwisho kabisa sasa yeye akaona awaadhibu kwa matakwa yake" tutakwenda juu zaidi, ndio haiwezekani hukumu kutolewa namna hii" amesema Rajabu Ali Saleh