- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WALIOAMBUKIZWA CORONA WAFIKIA MILIONI 1 DUNIANI
Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona duniani kwasasa imefikia watu milioni moja ishara ya kupanda kwa kasi kiwango cha maambukizi ndani ya kipindi cha wiki chache zilizopita
Katika muda wa wiki moja iliyopita visa vingi vya virusi vya Corona vimerikodiwa duniani ikilinganishwa na muda wa karibu miezi mitatu tangu virusi hivyo vilipogunduliwa kwa mara ya kwanza.
Takwimu zilizikusanywa pia zinaonesha idadi ya vifo imefikia watu 51,178 ambayo ni maradufu ya vifo vilivyorikodiwa hadi tarehe 27 mwezi Machi.Bara la Ulaya ndilo kitovu cha virusi vya Corona ambako mataifa ya Italia na Uhispania yameathirika zaidi kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi na vifo vitokanavyo na ugonjwa wa COVID-19.
Hata hivyo kumekuwa na ishara ya kupungua kiwango cha maambukizi nchini Italia kutoka asilimia 18 hadi asilimia 5 ya visa vinarikodiwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita.