Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 11:43 pm

NEWS: WALIMU WATATU WAUWAWA NA AL SHABAAB NCHINI KENYA

Walimu watatu wamepigwa risasi hadi kufa na Kundi la Wanamgambo wa Al Shabaab katika mji wa Garisa kaskazini mwa Kenya katika mpaka wa Kenya na Somalia.

Image result for al shabab attack kenya"

Huku kituo cha polisi kikichomwa moto na mfumo wa mawasiliano wa Safaricom kuharibiwa vibaya katika eneo la Kamuthe mapema leo asubihi.

Washambuliaji hao waliharibu mawasiliano kabla ya kutoroka.

Maafisa wa Jeshi la polisi nchini Kenya wanafuatilia kwa karibu chanzo cha wavamizi hao huku ripoti za kiusalama zikionyoesha kwamba wavamizi wameweka vilipuzi chini ya ardhi katika barabara ya eneo hilo.

Kenya imekuwa katika hali ya tahadhari baada ya kupata taarifa za kijasusi kwamba kundi la Al Shabab linapanga kufanya mashambulio zaidi.

Shambulio Garissa

Hili ni shambulizi ya 11 kutekelezwa na kundi la Al Shabab nchini Kenya katika kipindi cha wiki 6. Mashambulizi 4 yakitekelezwa Garissa, 3 Wajir, 2 Mandera na 2 Lamu.

Shambulio Garissa

Eneo la Mawasiliano lililoharibiwa na wanamgambo hao.