Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 7:27 pm

NEWS: WALEMAVU WAILILIA SERIKALI.

DODOMA: WALEMAVU waishio katika kata ya Hombolo manispaa ya Dodoma wameiomba serikali kuzichukulia hatua kali taasisi, mashirika na watu binafsi wanao jinufaisha na mali za watu wengine.

Kilio hicho kimetolewa wakati walemavu hao walipokuwa wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Hombolo wakati wakitambulishwa mradi wa utetezi kwa watu wenye ulemavu na ushiriki wa michakato ya serikali kwa ngazi za mitaa.

Peter Mabwayi ambaye ni mlemavu wa viungo mkazi wa Hombolo (B) amesema kuwa kuna mashirika,taasisi na watu binafsi ambao wamekuwa wakitumia kigezo cha ulemavu wao kujipatia fedha wakati wao wakiendelea na kuteseka na umasikini zaidi.

Hata Hivyo kupitia mradi huo wameiomba serikali kuzichukulia hatua stahiki kwa kuwa niuonevu kutokana na tabia hiyo ambayo wanayotumia ya kutumia hali zao kujipatia mamilioni ya fedha.

Kwa upande wake mwezeshaji wa uundaji wa klabu za vijana Jaruo Karebe kwenye mradi huo,ambao umefadhiriwa na shirika lisilo la kiserikali la Foundation Civil Society,amesema lengo la uundaji ni kuwapatia mikopo ili waweze kuondokana na utegemezi.

Sambamba na hayo Katibu wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu mkoa wa Dodoma Justus Ng’wantalima amewataka wazazi na walezi wenye watoto ambao ni walemavu wahakikishe wanawasomesha kwa elimu ya kutosha.