Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:51 am

NEWS: WAKULIMA WALIA NA BAJETI YA SERIKALI.

DODOMA: JUKWAA la Wakulima Wanawake wadogowadogo Tanzania limeiomba Serikali kuongeza bajeti ya kilimo ili kuweza kuleta tija kwa mkulima mdogo kutokana na kutofikiwa na pembejeo za kilimo,lengo kuweza kufikia uchumi wa kati wa viwanda .

Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Dodoma na Rais wa Jukwaa hilo Tanzania, Amina Senge wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano mara baada ya Kikao cha ushawishi na utetezi wa rasilimali ikiwemo ardhi na miradi ya maendeleo ya wakulima wanawake wadogo kilichoandaliwa na Shirika la Action Aid Tanzania.

Aidha amesema kuwa kumekuwepo na mapungufu katika bajeti ya kilimo kutokana na matumzi ya ndani ya bajeti kuwa juu kuliko fedha za maendeleo.

Naye Sofia Bhoke Mkulima Mdogo amesema kuwa Serikali imekuwa na sera nzuri lakini utekelezaji ngazi za chini hakuna hususani katika pembejeo za kilimo.

Kwa upande wake Dokta Honga toka Wizara ya Kiimo,mifugo na uvuvi akatoa ufafanuzi kuhusiana na suala la pembejeo za Kilimo.