- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAKULIMA WAITAKA SERIKALI KUTOA ELIMU KWA WANANCHI JUU YA UHIFADHI NA UTUNZAJI WA MAENEO YAO
DODOMA: WAKULIMA wadogo wadogo wameita serikali kuhakikisha inawaelimisha wananchi juu ya uhifadhi na utunzaji wa maeneo yao badala ya kuwahamisha kinguvu.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Mwenyekiti wa bodi ya mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA)VERONICA SOPHU wakati wa kongamano maalumu lenye lengo la kujadili changamoto zinazowakabili wakulima wadogo kutoka katika meeneo mbalimbali nchini.
Bi. SOPHU amesema kuwa ili kufikia uchumi wa kati na wa viwanda serikali inatakiwa kuwaelimisha wananchi hususani wakulima kuhusiana na kulimo wanacholima katika maeneo yao pamoja na kuwapatia maeneo ya kutosha.
Amesema kuwa wakulima ndio watakaofanikisha zoezi la kufikia uchumi wa kati wa viwanda kwani asilimia kubwa ya viwanda inategemea kilimo hivyo kuwa wakulima katika maeneo ya waliyokuwa wakilima toka mwaka 1970 na kuyafanya kuwa maeneo ya hifadhi ni sababu mojawapo inayodidimiza kulimo nchini.
Veronica Sophu amesema endepo serikali ikiendelea na utaratibu wa kuwaondoa kinguvu wakulima katika maeneo yao ya asili kwaajili ya kupisha hifadhi za taifa, Tanzania haitawezekana kufikia Tanzania ya viwanda.
Waziri wa kilimo ,mifugo na uvuvi,DK.CHARLES TIZEBA,amesema serikali haiwezi kuacha hifadha za taifa zikiendelea kuharibiwa na kuwa serikali haipendi kuona wakulima wakinyanyasika hivyo wakulima wanatakiwa kufuta sheria za uhifadhi na utunzaji wa mazingira.Lengo la Kongamano hilo nikuimarisha mawasiliano na kuwaunganisha wakulima wadogo kupitia vikundi na mitandao yao katika ngazi mbalimbali ili kujenga mtandao wa kitaifa wenye nguvu yakumuwezesha mkulima.