- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAKILI WA SABAYA AWEKA PINGAMIZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI
Arusha. Wakili wa utetezi, Fridolin Gwemelo katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya na wenzake sita ameweka pingamizi la kupokelewa kama kielelezo cheti kilichowasilishwa mahakamani na shahidi wa saba wa jamhuri ambaye ni ofisa wa Tehama wa benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Jofrey Abimael Nnko.
Cheti hicho kinaonyesha Sabaya na wenzake walivyorekodiwa katika benki ya CRDB tawi la Kwa Mrombo, Januari 22 kati ya saa 10:09 hadi saa 11:05 ambacho kilikabidhiwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Wakili Gwemelo ambaye anawatetea mshitakiwa wa tatu na nne katika kesi hiyo, mbele ya hakimu mkazi, Patrisia Kisinda amenieleza mahakama kuwa, cheti hicho hakionyeshi ubora wa vifaa na mfumo uliotumika.