Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 6:40 pm

NEWS: WAKILI FATMA KARUME KUKATA RUFAA ADHABU YA KUPOKONYWA UWAKILI

Wakili wa Tanzania fatma karukme aliyevuliwa uwakili siku ya Ijumaa ameapa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo alioutaja kua kinyume na sheria.

Akizungumza kwa njia ya simu na BBC Bi karume alisema kwamba Jaji wa mahakama aliyetoa uamuzi huo hakufuata taratibu yoyote kabla ya uamuzi huo huo.

Tokeo la picha la fatma karume na waandishi

Alisema kwamba pia atakwenda katika kamati ya mawakili ili kutoa malalamishi yake kuhusu uamuzi huo ambao anasema kwamba unakiuka haki zake za kisheria.

Hakunipa haki yangu ya kusikilizwa , hakunipa notisi yoyote ili kusikiliza malalamishi kuhusu wakili wangu , amevuruga kabisa sheria, alisema bi karume ambaye ni ,mtetezi wa haki za kibinaadamu mbali na kuwa wakili wa kikatiba.

''Eti pia kaamua kwamba Ado Shaibu amlipe fidia rais Magufuli inawezekanaje hiyo ilihali rais anatetewa na wakili mkuu ambaye analipwa na kodi ya mwananchi''.

Hatahhivyo wakilki huyo amesema kwamba hashangazwi na uamuzi uliotolewa kwa kua hata aliyekuwa mbunge wa singida mashariki Tundu Lissu hakupatia haki yake alipowasili mahakamani kuomba haki yake.

''Katika sheria kama umetoa kauli zinazolalamikiwa na serikali ni lazima upewe notisi uende kujitetea, useme ni kwa nini umesema mambo hayo nayo serikali iseme ni kwa nini kauli hizo hazihitajiki , lakini mimi sijapewa haki hizo fesheli kaamua alivyootaka''.

Siku ya Ijumaa wakili huyo alisimamishwa kufanya kazi za uwakili katika eneo la Tanzania bara.

Maamuzi hayo yametolewa na Jaji Feleshi kwenye kesi iliyofunguliwa na mwanaJF Ado Shaibu akipinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG).

Mahakama Kuu imeamuru Fatma apelekwe kamati ya maadili kwa madai ya kushambulia ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

Sababu yake ilitajwa kuwa kile alichokizungumza katika kesi iliofunguliwa na katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano katika chama cha Wazalendo, Ado Shaibu kupinga uteuzi wa Mwanasheria mkuu wa serikali Dkt Adelarus Kilangi aliyeteuliwa na rais John Pombe Magufuli mnamo February Mosi 2018.