Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 4:33 pm

NEWS: WAKILI AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUFANYA KAZI KWA KUFUATA MISINGI BILA KUJALI MATAMSHI YA VIONGOZI

DODOMA: WATUMISHI wa Serikali nchini wametakiwa kufanya kazi zao kwa kufuata misingi na taratibu za utumishi badala ya kufanya kazi kwa matamshi ya viongozi hususani kauri za rais.

Hayo yameelezwa na wakili wa Kujitegemea Kuwayawaya .S.Kuwayawaya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa.

Wakili huyo amesema kuwa kuna tatizo kubwa kwa watumishi wa serikali kushindwa kufanya kazi kwa nia ya kusimamia misingi ya utumishi na taratibu zake na badala yake wamekuwa wakijificha katika matamshi ya rais kwa kuonesha wazi kuwa kazi zao wanazifanya kwa uoga.

Kiongozi huyo mbali na kutaka watumishi wa serikali kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kazi badala ya kujificha katika kivuli cha makamko ya rais amewataka wasaidizi wa rais kumsaidia kuwa kauli anazozitoa zinakuwa na maelekezo ambazo haziwezi kupelekea kuwepo kwa mashaka licha ya kuwa zinaweza kupingwa.

Wakili Kuwayawaya amesema amelazimika kuzungumza na vyombo vya habari kwa lengo la kutoa hisia zake kabla ya kusimikwa kuwa Makamu askofu wa kanisa la Angalikana la Kiinjili Tanzania (KAKT) na huduma ya Global Revival Network na ibada hiyo itafanyika jumapili katika ukumbi wa Tangamano ulioko Mvumi Makulu wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Aidha amesema viongozi waliopewa dhamana ya kulinda raia na mali zao,wajitahidi kufanya kazi zao kwa kufuata taratibu,sheria na maadili ya kazi zao.

“Mfano polisi anapomuonea raia raia afanye nini,mtendaji wa kata au kijiji anaposhindwa kumuhudumia raia ipasavyo raia afanye nini,ikumbukwe kuwa binadamu ni mnyama kama mnyama mwingine hakifikishwa mahali mahali ambapo hawezi kuvumilia,kumrudisha katika hali ya kawaida ni ngumu sana”alisema Kuwayawaya.

Hata hivyo amesema kuwa viongozi ambao wamekuwa wakitoa matamshi ambayo yana viashiria vya uchochezi kwa viongozi waliopo madarakani ni vyema wakajirekebishaili kuondokana na machafuko ambayo yanaweza kujitokeza.

“Kwa upande wa Serikali ingekuwa vyema vile vikosi vya inteligensia vya polisi,Jeshi na hata wote wenye jina hilo wapewe uwezo wa kufuatilia matukio ya uvunjifu wa amani na kuyazuia huko huko kabla hayajajulikana” alisema Wakili Kuwayawaya.

Akizungumzia suala ya nchi ya viwanda,Wakili Kuwayawaya amesema kuwa serikali inatakiwa iliangalie upya swala la Shirika la Viwanda vidogo Vidogo(SIDO) ili kupanua huduma na kuziboresha ili vijana wanaomaliza vyuo waingie katika kubuni,kuanzisha na kuendesha viwanda vidogo vidogo.

Pia amesema serikali inatakiwa kupanua nafasi za jeshi la kujenga taifa na vyuo vya ufundi ili ikiwezekana vijana wakitoka shule kidato cha nne na cha sita wote waingie katika jeshi la kujenga taifa mwaka mmoja,Veta mwaka mmoja na baada ya hapo waende vyuo vikuu ili kule wanaposoma muda wa likizo wafanye mazoezi ya ufundi waliosomea katika taasisi za serikali na za binafsi.

Wakili Kuwayawaya ambaye 30 Julai anatarajiwa kusimikwa kuwa askofu wa huduma ya Global Revival Network,huduma ambayo inafanya kazi na madhehebu yote,yaani Interdenominational kwa lengo la uamsho wa Kiroho Duniani, alisema ni vyema madhehebu yote kushikamana na kuliombea taifa na dunia kwa ujumla ili watu waweze kushikamana.