- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAKAZI WA NHOLI DOM WAMLILIA MAGUFULI
DODOMA: Wakazi wa kijiji cha Nholi wilayani Bahi mkoani Dodoma wamemuomba Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuufungia mgodi wa machimbo ya Dhahabu ulipo kijijini hapo kutokana na kuendeshwa kinyume cha kanuni za madini na kuipotezea serikali mapato.
Mgodi wa Machimbo ya dhahabu wa Nholi wilayani Bahi mkoani Dodoma umekuwa ukilalamikiwa na wananchi wa kijiji cha Nholi kutokana na uendeshwaji wa mgodi huo ambao ulianza kuendeshwa bila kuishirikisha serikali ya kijiji hicho pamoja na kuwa ardhi ni ya wananchi.
Wakizungumza wakati wa mkutano wa hadhara baadhi ya wananchi wameiomba serikali kuingilia kati katika kuhakikisha kuwa mgodi huo unasimamisha shuguli zake hadi hapo utaratibu utakapo badilishwa kwani licha ya kuwepo kwa mgodi huo wakazi hao hawanufaiki na chcohote
Akijibu malalamiko hayo kwa niaba ya serikali afisa mtendaji wa kijiji hicho Augustino Apolinary, amesema ipo timu iliyoundwa kuja kuona jinsi gani inaweza kuufanyia marekebisho mfumo ulipo hivi sasa ili kijiji kipate haki yake
Juhudi za kuwapata wamiliki wa mgodi huo wa dhahabu ziligonga mwamba
Sekta ya madini ikiwemo migodi ya dhahabu imekuwa ikiliingizia pato kubwa serikali ambapo kwa hivi sasa serikali ya awamu ya tano imeanza kupambana na mianya ya wizi na utoroshwaji wa madini ndani ya nchi