- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAKAZI WA NAIROBI NA MOMBASA WAWEKEWA MARUFUKU KUTOTOKA NJEE
Serekali nchini Kenya imeongeza sheria kali zaidi ya kupambana na ugonjwa wa Corona sasa Wakaazi wote wa Maeneo ya jijini Nairobi na Old towm mjini Mombasa nchini Kenya hawatoruhusiwa kutoka katika maeneo yao katika kipindi cha wiki mbili zijazo kuanzia leo Jumatano saa moja usiku Mei 6, 2020.
Hatua hiyo inalenga kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona katika maeneo mengine ya miji ya Nairobi na Mombasa huku wagonjwa wengine wapya 47 wakitangazwa na kufanya idadi ya maambukizi kufikia watu 580.
Akizungumza na vyombo vya habari Waziri wa Afya Mutahi kagwe amesema kwamba kati ya wagonjwa hao 47, 32 wanatoka Mombasa huku 11 wakitoka Nairobi.Amesema mtaa wa Bondeni ambao wakaazi wake wamekuwa wakiuka masharti ya afya yaliotolew na serikali una wagonjwa 18 wapya huku mtaa wa Estleigh ukiripoti wagonjwa 5 wapya.