- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAJERUMANI WAINGIA UWANJANI KUPIGA KURA LEO KULICHAGUA BUNGE
Germany: Leo tarehe 24 Septemba ,Wajerumani wanapiga kura katika uchaguzi mkuu, ambapo kiongozi wa chama cha Christian Democratic -CDU Kansela Angela Merkel anawania kuchaguliwa tena kwa muhula wa nne wa kipindi cha miaka minne.
Mpinzani wake mkubwa wa kiti cha Ukansela ni mkuu wa chama cha Social Democratic SPD, ambacho hadi uchaguzi huu kilikuwa mshirika katika serikali ya Muungano pamoja na CDU.
Wajerumani wanapiga kura leo Jumapili katika uchaguzi ambao unatarajiwa kushuhudia kansela Angela Merkel akishinda muhula wa nne wa kihistoria na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia kikitarajiwa pia kuingia bungeni kwa mara ya kwanza katika muda wa zaidi ya nusu karne.
mgombea wa chama cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto Martin Schulz wa chama cha Social Democratic SPD, amewahimiza wapiga kura jana Jumamosi kujitokeza na kupiga kura.
"Tunataka kuwapa hamasa zaidi ili tuweze kuwafikia watu wengi zaidi ," kansela mwenye umri wa miaka 63, alisema mjini Berlin kabla ya kuelekea kaskazini katika jimbo lake kwa ajili ya duru ya mwisho ya kampeni.