Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 2:30 pm

NEWS: WAJASILISMALI WATAKIWA KUFANYA KAZI ZAO KWA UBUNIFU

DODOMA: VIJANA ambao wanajishughulisha na ujasiliamali wametakiwa kufanya kazi zao kwa ubunifu zaidi sambamba na kuwa waaminifu katika jamii na kwa wateja wao.

Kauli hiyo imetolewa na Frank Mamba maarufu kwa jina la Mamba Pictures ambaye yeye anajihusisha na upigaji picha za video na Mnato mjini hapa.

Mamba alisema katika ujio wa Dodoma kuwa makao makuu vijana ambao wamafanya biashara mbalimbali kwa maana ya ujasiliamali wanatakiwa kuwa wabunifu huku wakifanya kazi zao kwa uaminifu ili kujitofautisha na wajasiliamali wa ukweli na matapeli.

Akizungumza na Tanzania daima Mamba alisema licha ya kuwa yeye ni mpiga picha wa picha za mnato na za video lakini amekuwa akijipambanua zaidi na watu wengine huku akitambua kuwa upigaji wake wa picha ndiyo ajira yake.

“Mimi natambua wazi kuwa kazi ya kupiga picha ndiyo ajira yangu na imenifanya kuishi mjini kwa kujitegemea kwa kuweza kupanga nyumba na kuishi bila tatizo mimekuwa nikiwasaidia jamaa na ndugu zangu pale inapotokea tatizo la kifamilia au lolote lile.

“Nguzo pekee ambayo nilijiwekea ni kuwa mwaminifu katika kazi zangu pamoja na kuwa mbunifu katika kazi zangu za picha pia mimekuwa najiepusha sana na kauli mbaya na kujenga mahusiano mazuri na jamii pamoja na wateja wangu.

“Kazi ya kupiga picha ina changamoto nyingi wakati mwingine jamii inaona kitendo cha kupiga picha ni sawa na kukosa kazi na wakati mwingine inatokana na kuwepo kwa watu ambao siyo waaminifu ambao wanapiga picha na kuchukua fedha ya mteja na hatimaye hapeleki kazi aliyopewa na kufikia kutoleana kauli mbaya kati ya mpigapicha na mteja husika” alieleza Mamba.

Alisema kwa sasa teknolojia inakuwa kwa kasi tofauti na ilivyokuwa awali na sasa watu wanataka kuona kitu kipya na chenye ubora hivyo kuna kila sababu ya kufanya kazi ambayo unajivunia ubora wake ili uweze kupata wateja wengi zaidi.

Mamba alisema katika kuiboresha kazi yake ya picha amefanikiwa kufungua ofisi yake ambayo ipo jamatini mjini hapa ambayo inamfanya kutambuliwa zaidi na kuweza kutoa ajira za muda mfupi kwa vijana.

Mamba alisema katika kuhakikisha anapata ajira kwa maana ya kujiajiri kwa sasa anafanya kazi ya upigaji picha kwa ubunifu mkubwa na sambamba na kujenga misingi ya uaminifu kwa jamii ili jamii iweze kutambua kuwa kazi hiyo ni sehemu ya ajira na inaweza kumpatia mtu kipato badala ya kukaa vijiweni na kuwa ombaomba au kujiingiza katika makundi ya kuhuni.