- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAHUJUMU UCHUMI 4 WAMUANDIKIA DDP BARUA KUKIRI MAKOSA YAO
Mkurugenzi na mwanasheria wa kampuni ya mawasiliano ya Six Telecoms Limited Ringo Tenga na wenzake nne wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi inatarifiwa kuwa wamemwandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) Biswalo Mganga wakiomba kukiri mashtaka yao.
Wakili wa Serikali, Patrick Mwita, Aprili 5, 2019 alidai mahakamani mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thoma kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na ofisi ya mashtaka inaandaa nyaraka ili kesi hiyo ianze kusikilizwa na Aprili 17 mwaka huu kesi hiyo iliitwa tena kwa ajili ya kusikilizwa.
Agosti 23 mwaka huu wakili wa serekali aliiomba mahakama ihairishe tena kesi hiyo kwa ajili ya kukamilisha nyaraka ili kesi hiyo iweze kuhamishiwa kwenye mahakama ya Mafisadi
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni pamoja na Hafidhi Shamte au Rashidi Shamte ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mkuu wa Fedha wa kampuni hiyo, Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms.
Washtakiwa hao ambao walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Novemba 20, 2017 wanakabiliwa na mashtaka sita likiwamo la utakatishaji fedha na hivyo kukosa dhamana hadi sasa.
Katika kesi ya msingi, Dk. Ringo, ambaye ni Mkurugenzi na Mwanasheria wa kampuni hiyo na wenzake wanadai kuwa kati ya Januari 1, 2014 na Januari 14, 2016 Dar es Salaam, walitoza malipo ya mawasiliano ya simu za kimataifa chini ya kiwango cha Dola 0.25 za Marekani kwa dakika kwa lengo la kujipatia faida.
Pia katika kipindi hicho, wanadaiwa kuhujumu miundombinu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kutoza gharama chini ya kiwango na kushindwa kulipa kiasi cha Dola 3,282,741.12 za Marekani kwa TCRA kama malipo ya mapato.
Pia washtakiwa hao wanadaiwa katika kipindi hicho walishindwa kulipa ada za udhibiti za Dola 466,010.07 za Marekani kwa TCRA.
Katika shtaka la utakatishaji wa fedha, Hafidhi, Noni, Tenga na Chacha, wanadaiwa kuwa walitumia ama walisimamia Dola 3,282,741.12 za Marekani wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya udanganyifu linalotokana na mashtaka yaliyotangulia.
Pia washtakiwa hao wanadaiwa kuwa waliisababishia TCRA hasara ya Dola 3,748,751.22 za Marekani (sawa na Sh bilioni nane).