- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAGONJWA 2 WAFARIKI KWA CORONA TANZANIA
Dar es Salaam. Wizara ya Afya nchini Tanzania imetangaza kutokea kwa vifo vya watu wawili, waliofariki dunia kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa corona (COVID 19) na kufanya idadi ya waliokufa kwa ugonjwa huo nchini Tanzania kufikia watatu.
Katika taarifa yake iliyotolewa leo na Waziri wa Afya nchini humo Bi Ummy Mwalimu amesema kuwa walioambukizwa ugonjwa huo nchini sasa wamefikia 32 baada ya wagonjwa wengine saba kuongezeka leo, wakiwemo wawili wa Zanzibar.
“Tunasikitika kutoa taarifa ya vifo viwili vilivyotokea leo miongoni mwa wagonjwa waliothibitishwa kuwa na maambukizi ya corona nchini.”
“Waliofariki dunia ni mwanaume mwenye umri wa miaka 51 Mtanzania mkazi wa Dar es Salaam tuliyemtolewa taarifa Aprili 8, 2020 na mwingine ni mwanaume mwenye umri wa miaka 57,” amesema Ummy.
Amesema wagonjwa hao watano, wanne ni wanaume wenye umri kati ya miaka 41 hadi 68 na mwanamke mmoja mwenye miaka 35.
“Leo Waziri wa Afya wa Zanzibar ametangaza uwepo wa wagonjwa wapya wawili waliothibitika kuwa na corona. Jumla ya waliothibitishwa kupata maambukizi ni 32. Kati ya hawa watano wamepona na wagonjwa wengine 24 wanaendelea vizuri na matibabu,” amesema Ummy.
Ameongeza, “vifo vimefikia vitatu tangu ugonjwa huu uliporipotiwa nchini. Kwa mara nyingine Serikali inaendelea kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huu kama tunavyowapatia taarifa na elimu mara kwa mara kupitia njia mbalimbali.”