- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAFUNGWA 45 WANARIPOTIWA KUFARIKI DUNIA NCHINI DRC
Wafungwa 45 wamefariki dunia katika gereza kuu la Bukavu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tangu mwanzo wa mwaka huu kwa kile walichodai kuwa ni kukosa huduma ya afya.
Gereza hilo lenye uwezo wa kupokea wafungwa kati ya 350 na 500 lililojengwa tangu enzi za ukoloni, lakini kwa sasa lina karibu wafungwa elfu mbili.
Wafanyakazi wa afya wanaofanya kazi katika gereza hilo, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamethibitisha taarifa hiyo.
“Wafungwa 45 wamepoteza maisha, tangu Januari mwaka huu kwa sababu ya ukosefu wa huduma ya afya”, mmoja wa wafanyakazi hao ambao hakutaja jina aliyenukuliwa na mwandishi wetu mjini Bukavu, William Basimike, amebaini.
Wengine walihamishwa katika Hospitali kuu ya mjini Beni, lakini hakukuwa na dawa na vifaa vya kuwasaidia kupata huduma hiyo.
Hali hii imesababisha wafungwa kugoma wakilalamikia ukosefu wa dawa na vifaa vya kufanya vipimo.