- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAFUGAJI WA MBWA WAPEWA SOMO.
DODOMA: Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya kichaa cha mbwa afisa Mifugo msaidizi wa manispaa ya Dodoma Innocent Peter ameitaka jamii kutumia maadhimisho hayo kwa ajili ya kuwapatia chanjo mbwa wao ili kuwakinga na ugonjwa huo.
Akizungumza na kituo hiki leo mjini Dodoma Peter amesema kuwa jamii inatakiwa Kutumia siku hiyo kwa manufaa makubwa maana ugonjwa huo ni hatari hata kwa binadamu.
Aidha amewataka wafugaji wa mbwa kufuata taratibu na sheria za ufugaji wa mifugo hiyo ikiwa ni pamoja na kuwafungia katika mabanda mbwa wote nyakati za mchana na kuwafungulia nyakati za usiku.
Amesema kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la mbwa wanaozulula mitaani hali ambayo ni hatari kwani iwapo mmoja akipata kichaa cha mbwa inakua rahisi kuwaambukiza wenzake na inaweza kusababisha madhara hata kwa binadamu.
Kwa mwaka 2016 Takwimu zinaonesha watu 1,600 hasa watoto hufa nchini kila mwaka kutokana na ugonjwa wa kichaa cha mbwa .
Kichaa cha mbwa duniani huadhimishwa September 28 mwezi wa 9 kila mwaka.