Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 11:26 am

NEWS: WAFUGAJI NCHINI WATAKIWA KUTUNZA MALISHO KUEPUKA CHANGAMOTO

DODOMA: Wafugaji nchini wametakiwa kuhakikisha wanaanzisha utaratibu mpya wa utunzaji wa malisho ili kuepuka changamoto mbalimbali zinazowakabili hususani nyakati za kiangazi.

Akizungumza katika kikao maalum cha wafugaji mkoani hapa katika ukumbi wa shule ya sekondari Omonga mjini DODOMA afisa mifugo mkuu kutoka wizara ya kilimo mifugo na uvuvi Bw SIMON LYIMO Amesema wafugaji wanapaswa kutumia mbinu za kisasa za kukuza mifugo yao kwa kutumia mfumo wa uoteshaji wa malisho ya mifugo ili kunufaika zaidi katika ufugaji wenye tija .

Kwa upande wake MKURUGENZI WA KAMPUNI YA MADAWA YA MIFUGO [TANZANIA LIVESTOCK COMPANY LIMITED]] BW. ERNEST TARIMO amewasisitiza wafugaji wa Tanzania wotejuu ya kutoa na Ushirikiano katika kufanya kazi kwa lengo la kuleta maendeleo kupitia ufugaji

Naye mwenyekiti wa wafugaji kanda ya magharibi mkoa wa KATAVI KUSUNDWA WAMALWA amewataka wafugaji kuwa na bodi ambayo itasaidia kuingia mkataba na Makampuni pamoja na kuweka utaratibu mzuri ambao utawasaidia kufanya kazi kwa bidii ikiwemo kuwaalika wakurungezi wa makampuni katika mikutano wa wafugaji