- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAFANYAKAZI WA SEREKALI ZIMBABWE WAANDAMANA KUDAI MALIPO
Wafanyakazi wa serekali nchini Zimbabwe wameandamana leo Jumatano baada ya serekali kushindwa kuridhia madai yao ya kutaka walipwe mishahara inayokwenda sambamba na thamani ya dola za Kimarekani.
Polisi waliruhusu vyama vya wafanyakazi kufanya maandamano hayo ya kudai mishahara bora, jambo ambalo linatizamwa na wadadisi kama mtihani kwa rais Emmerson Mnangagwa, ambaye siku za hivi karibuni alipiga marufuku maandamano ya upinzani.
Serikali imesema haina uwezo wa kulipa mishahara inayofuatana na thamani ya dola ya Marekani, hali ambayo itapelekea mfanyakazi anayepokea mshahara mdogo kulipwa dola ya Zimbabwe elfu 7,293, sawa na dola za Marekani 475 kwa mwezi, kuliko dola ya Zimbabwe 1,023 anazolipwa sasa.
Wafanyakazi wa Zimbabwe wanaathirika kutokana hali mbaya ya uchumi wa taifa, inayosababishwa kwa kiasi kikubwa na mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu, uhaba wa sarafu za kigeni, mafuta na dawa, pamoja na mgao wa umeme ambao unazorotesha shughuli za viwanda na uchimbaji madini.