Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 4:46 am

NEWS: WAFANYAKAZI HEWA WA TIGO WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Matapeli wanaojitambulisha kama wafanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo wamefikishwa Katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kwa makosa ya kudukua taarifa za wateja wa huduma ya kifedha ya TigoPesa inayotolewa na kampuni hiyo.

Matapeli hao ambapo wamekuwa wakiwatapeli wateja wa kampuni ya Tigo kwa kujitambulisha kama wafanyakazi halali wa Tigo wakati kiukweli sio waajiriwa wa Tigo.

Washtakiwa hao wamepandishwa kizimbani tena leo Agosti 6, 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salim Ally.

Matapeli hao utumia mbinu hiyo kujipatia taarifa za siri za wateja hao ambazo baadae wamezitumia kuiba kiasi cha fedha zipatazo shilingi milioni 26 kutoka kwa wateja mbalimbali wa mtandao huo kupitia huduma ya Tigo Pesa


Waliofikishwa mahakamani ni Raia wa Burundi, Hamis Singa (30) ambaye anajitambulisha kama kiongozi wa wafanyakazi wa Tigo mjini Babati na wenzake wanne (si wafanyakazi wa kampuni hiyo) ambao wanatuhumiwa kujipatia Sh milioni 26 kutoka kwa wateja wa Vodacom na Airtel kwa njia ya ulaghai.

Wengine ni wafanyakazi watatu wa Tigo Mlimani City na wenzao wawili (si wafanyakazi wa kampuni hiyo) ambao wanadaiwa kujipatia zaidi ya Sh milioni 20 na kutakatisha fedha hizo huku wakijua ni zao la uhalifu.

Wakisomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, ilidaiwa washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka saba likiwemo moja la kutakatisha fedha.