- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WADHAMINI WATAKA TUNDU LISSU KUKAMATWA
Dar es Salaam. Wadhamini wa aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki,(Chadema) Tundu Lissu leo tarehe 20 Februari 2020, wamewasilisha maombi mahakamani ya kuitaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya Jijini Dar es salaam kuitaka itoe HATI ya Kumkamata mdhaminiwa wao (Tundu Lissu).
Kama unakumbuka Desemba 19, 2019 Mahakama hiyo ilitoa amri kwa wadhamini hao kuhakikisha mshtakiwa huyo anafika mahakamani tarehe itakayopangwa.
Wadhamini hao ambao ni Ibrahim Ahmed na Robart Katula, wameieleza mahakama leo kwamba, juhudi zao za kumfikisha mahakamani hapo Lissu, aliyekuwa Rais wa TLS anakabiliwa na kesi ya uchochezi katika mahakama hiyo,
Lissu hakuonekana mahakamani Jumatatu ya Januari 20, 2020, huku wadhamini wakitakiwa na mahakama kuhakikisha anarejea nchini ili kuendelea na kesi yake. Januari 30, 2020 Robert Katula ambaye ni mdhamini wa Lissu aliieleza mahakama hiyo kuwa juhudi walizofanya ni pamoja na kuwasiliana na mshtakiwa bila mafanikio pamoja na kumuandikia barua mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuwasaidia ili Lissu arejee nchini.
Maombi ya wadhamini hao, yamefikishwa wakati shauri hilo lilipotajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Awali, wakili wa serikali mwandamizi Wankyo Simon, amedai upande wa mashtaka umepokea maombi kutoka kwa wadhamini wa mshtakiwa huyo, ya kuomba kumkamata ili waweze kujitoa kwenye udhamini huo. Wankyo amedai, upande wa mashtaka umeridhia kusikilizwa maombi hayo, ambapo wameomba yasikilizwe kesho tarehe 21 Februari 2020.
“Shauri hili limekuja kwa ajili ya kutajwa limekuwa likikwama kutokana na mshtakiwa wa nne kutokuwepo na leo tumepokea maombi namba mbili ya mwaka 2020 yaliyowasilishwa na wadhamini wakiiomba mahakama itoe kibali cha kumkamata mshtakiwa,” amedai wakili Wankyo na kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine ili maombi hayo kusikilizwa"
Katula amedai kuwa, wameshindwa kumkamata na kumleta mshtakiwa huyo kwa nguvu zao, hivyo wanaomba kusikilizwa kwa maombi hayo. Baada ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Simba amehairisha shauri hilo kesho, ambapo pande zote zitakuja kuangalia taratibu za kisheria juu ya maombi hayo na kusisitiza kuwa, amri za kesi ya msingi bado zinaendelea kuwa na nguvu.
Mbali na Lissu, washtakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Simon Mkina, ni mhariri wa gazeti la MAWIO; Jabir Idrissa, mwandishi wa gazeti hilo na Ismail Mehbob, mfanyakazi wa kampuni ya uchapishaji ya magazeti ya Jamana.
Wanakabiliwa na mashitaka matano katika mahakama hapo, likiwamo uchochezi. Wote wanne, wanatuhumiwa kuandika, kuchapisha na kusambaza taarifa hizo kwenye gazeti la MAWIO la tarehe 14 Januari 2016, kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002. Habari ambayo inadaiwa kuwa ya uchochezi, ilibeba kichwa cha maneno kisemacho: “Machafuko yaja Zanzibar.