Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 11:15 pm

NEWS: WADAU WACHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI KISARAWE.

KISARAWE: Wadau mbalimbali wamejitokeza kuchangamkia fursa za uwekezaji wilayani Kisarawe wakati wa uzinduzi wa kongamano la fursa za uwekezaji wilayani humo.

Katika kongamano hilo limehudhuriwa na Wafanya biashara na taasisi mbalimbali ambao wameweza kufahamu fursa nyingi ambapo hapo awali walikuwa hawajui mazuri hayo.

Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano hilo, Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mhe. Selemani Jafo ameeleza kwa undani mpango wa serikali wa viwanda sambamba na kueleza kwa kina fursa zipi zilizopo Kisarawe.

Jafo ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa maelekezo yake kwa DAWASA aliyo yatoa miezi michache iliyopita ya kupeleka maji Kisarawe na eneo la uwekezaji wa viwanda ambapo mpango huo utachochea viwanda katika eneo la Visegese lililotengwa kwaajili ya viwanda.

Katika eneo hilo kwasasa kuna zaidi ya ekari 1000 zilizopimwa na kuchongwa barabara na viwanja 291 vya uwekezaji wa viwanda vikubwa na viwanda cha kati vimeshapimwa na kutengwa tayari kwa uwekezaji.

Aidha Mpaka sasa tayari viwanda vinane vimeshajengwa ikiwa pamoja na bandari kavu iliyopo itakayosaidia uwekezaji wa kisasa kutokana na kupitiwa kwa reli mbili za TAZARA na Reli ya kati.