- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WADAU WA AFYA WATAKIWA KUTUMIA TAKWIMU KWA USAHIHI.
DODOMA: Utumiaji sahihi wa Takwimu mbalimbali zinazohusu masuala ya afya, umetakiwa kuzingatiwa na kufanyiwa kazi ipasavyo ili kuleta mapinduzi chanya katika sekta hiyo nchini.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainabu Chaula, wakati akifunga kongamano la tatu la mwaka la kufuatilia na kutathmini masuala ya afya jijini Dodoma.
Amesema utumiaji huo wa takwimu kwa wadau wa Afya unatakiwa kuja na matokeo ya mtizamo tofauti na si kurudia mada zilizopita, katika mkutano mwingine kama huo unaotarajia kufanyika tena mwakani 2020:
Awali Akitoa taarifa mbele ya Mgeni Rasmi, Kaimu Mkuu wa Utawala na Management ya chuo kikuu cha Mzumbe Dkt. Eliza Mwakasangula, amesema tafiti zinatakiwa kufanyika na kuleta majibu juu ya namna bora ya kuimarisha na kujenga mifumo ya kuchakata taarifa juu ya huduma za afya nchini.
Dkt. Mwakasangula amesema vituo vya afya kumiliki miradi na taarifa kwa matumizi yao wenyewe ni moja ya nguzo za kuboresha taarifa zinazokusanywa na kuzitumia katika kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati muafaka.
Kongamano hilo limeandaliwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe, kwa kushirikiana na Chuo cha Mt. Fransisco cha Nchini Marekani, na kushirikisha wadau mbalimbali kwa kwa lengo la kufuatilia na kutathimini masuala ya afya.