Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 1:51 am

NEWS: WADAIWA KODI YA ARDHI KUPELEKWA MAHAKAMANI

DODOMA: WIZARA ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Kanda ya kati,imeanda Hati 500 za madai kwaajili ya kuwapeleka Mahakamani baadhi ya watu wanaomiliki ardhi ambao hawajalipa kodi hiyo.

Hayo yameelezwa leo Mjini Dodoma na Mwanasheria wa Wizara ya Ardhi Kanda ya Kati,JANE KAPONGO wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukusanyaji kodi za Ardhi.

KAPONGO amebainisha kuwa wameamua kufanya hivyo kutokana na baadhi ya watu wanaomiliki Ardhi kutolipa kodi hasa katikamiaka iliyopita.

Aidha Mwanasheria huyo amefafanua kuwa hivi sasa kuna madai 200 yamefunguliwa katika Mahakama ya Ardhi ambapo kati ya madai hayo kesi 98 zinaendelea huku wengine tayari wameshalipa madeni yao.

Hata hivyo amesema kuwa hivi sasa wana mkakati wa kupita kwenye Mitaa yote ya Manispaa ya Dodoma kwaajili ya kuwatangazia wale wote wanaodaiwa kodi hizo kwenda kuhakiki majina yao kwa hiari ili waende kulipa kodi.

Kwa upande wake Kamishna msaidizi wa Ardhi kanda ya kati,HEZEKIEL KITILYA amesema kuwa hivi sasa kodi za Ardhi zitalipwa kwa mfumo wa njia ya mitandao ya simu kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma.


Hata hivyo lengo amesema huduma hiyo mpya ya ulipaji wa kodi ya Ardhi kwa njia ya mtandao itawewezesha wananchi kuondokana na usumbufu wa kutembea kufuata huduma ilipo.