Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 9:27 pm

NEWS: WACHEZAJI WA SENEGAL WAZAWADIA MIL 200

Rais Macky Sall wa Senegal amewazawadia wachezaji wa timu ya taifa wa nchi hiyo zawadi ya Dolla $87,000 sawa na zaidi ya Tsh milioni 200 sambamba na mashamba kwa kila mchezaji moja kufuatia kufanikiwa kunyakuwa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Viwanja hivyo vipo katika mji mkuu, Dakar, na katika mji jirani wa Diamniadio wakati wa sherehe iliyofanyika ikulu ya rais.

Rais Macky Sall pia aliteua timu hiyo katika Tuzo ya heshima kutoka kwa Rais ambayo ni maarufu nchini Senegal, huku mashabiki wakishangilia nje ya lango.

Rais hapo awali aliishukuru timu hiyo kwa kufika “kilele cha dimba hilo la Afrika” na kuleta ”fahari na heshima ambayo inaashiria watu wa kipekee. ”

Pia alimsifu kocha wa timu hiyo, Aliou Cissé.

Senegal ilifanikiwa kumahinda Misri kwa mikwaju ya penalti 4-2, na kuwa mabingwa wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika historia yao.