Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 4:32 pm

NEWS: WACHAKACHUAJI WA MAFUTA YA PETROLI NCHINI WABANWA

DODOMA: Serikali imefanikiwa kudhibithi uchakachuaji wa mafuta ya petroli kutoka asilimia 87 kwa mwaka 2007 hadi kufikia chini ya asilimia 5 kwa mwaka jana, ambapo pia imesema imeanza ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta ili kuzuia ukwepaji wa kodi.

Hayo yamesema na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura),Felix Ngamlagosi mjini Dodoma wakati wa uzinduzi wa sekta ndogo ya mafuta ya petrol kwa mwaka 2016 ambapo uzinduzi huo ulifanywa msimamizi wa sekta ndogo ya matuta Inoccent Ruoga mjini Dodoma kwa niaba ya waziri wa nishati na madini Prof. Sospeter Mhongo.

Alisema kupungua kwa uchakachuaji huo unatokana na uwekwa kwa vinasaba ambavyo husaidia kugundua mafuta yaliyochakachuliwa hivyo kupunguza hasara kwa nchi na kwa watumiaji kwa kiasi kikubwa ambapo pia alisema iwapo serikali itafanikiwa kujenga mabomba ya mafuta serikali itaokoa zaidi mapato yanayopotea.

Pia alisema serikali imeweka vipaumbele katika usimamizi wa uuzaji na ununuzi wa mafuta ya petroli ili kuzuia ongezeko la bei za mafuta nchini ili iendane na bei ya soko la mafuta la dunia na kuongeza kuwa wameweza kutoa jumla ya leseni 1352 kwa vituo mbalimbali hapa nchi.

Alisema kwa mwaka huu seriakli imeweka vipaumbele katika ujenzi wa vituo vya mafuta maeneo ya vijijini, huku wakiendelea kukusanya takwimu sahihi za mafuta na kuhakikisha wadau wanauza na kununua mafuta kulingana na misingi ya iliyowekwa.

Alitaja baadhi ya changamoto ambazo wanakutana nazo kuwa ni kuwepo kwa upitishwaji wa mafuta ya magendo, kukosekana kwa miundombinu ya kisasa ya usafirishaji wa mafuta ,kukosekana kwa viwango vya mafuta na gesi na kutokuwepo kwa mabomba ya usafirishaji wa mafuta.