- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WABUNGE WENGINE 2 WA CHADEMA WAENDELEA KUSOTA RUMANDE
Wabunge wawili wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Peter Lijualikali wa Kilombero na Suzan Kiwanga na wenzao saba wemefikishwa Mahakamani na Kurudishwa Rumande hadi mwezi machi 1, 2019 Mahakama itakaposikikiliza ombi la kupinga dhamana yao lililowasilishwa na upande na Jamhuri.
Washitakiwa hao mwaka jana walipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza walikuwa 13 na kusomewa mashtaka nane likiwemo la kuchoma moto ofisi ya Serikali ya kijiji cha Sofi wilayani Malinyi. Hata hivyo Mahakama iliwaachia huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuwasilisha ushahidi wa kutosha ili kuwatia hatiani kabla ya Serikali kufufua tena kesi hiyo.
Jana mbele ya hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa Morogoro, Elizabeth Nyembele wakili wa Serikali, Edger Bantulaki aliwasilisha ombi la kupinga dhamana ya washtakiwa hao kutokana na baadhi ya washtakiwa hawajapatikana hivyo dhamana inaweza kukwamisha upatikanaji wa washtakiwa wengine. Wakili wa utetezi, Josephine Jackson alisema: “Baada ya kupata pingamizi tutawasilisha majibu ya hoja za pingamizi hilo la Serikali na kesi itatajwa tena Machi Mosi.”